Pages

Subscribe:

Monday 19 January 2015

Wahoji utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete



Wadau wa maendeleo mkoani Iringa, wameitaka Serikali itekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kutengeneza Barabara ya Iringa-Msembe (Hifadhi ya Taifa ya Ruaha) yenye urefu wa kilomita 114 kwa kiwango cha lami ikiwa ni jitihada za kukuza uchumi wa mikoa ya Kusini.
Walitoa ombi hilo jana kwenye kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Iringa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Siasa ni Kilimo, Manispaa ya Iringa.
Wadau hao waliamua kuunda timu maalumu itakayokutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda au Rais Kikwete kwa ajili ya kuwasilisha ombi maalumu la kuharakisha ujenzi huo. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Steven Mhapa alisema ubovu wa barabara hiyo umeendelea kuzorotesha sekta ya utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamudu Mgimwa alisema Mkoa wa Iringa unapaswa kuwa na mkakati wa kuzipigia debe barabara zote zinazobeba uchumi wa nchi kama ilivyo kwa barabara hiyo ya Hifadhi ya Ruaha.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Profesa Peter Msolla alisema mbali na kuikuza sekta ya utalii mkoani Iringa, kujengwa kwa kiwango cha lami kwa barabara hiyo kutachochea uanzishwaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi zenye uhusiano na sekta hiyo na hivyo kusaidia kuongeza ajira hususani kwa vijana.
Awali, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Iringa, Paul Lyakurwa alisema baada ya Rais Kikwete kutoa ahadi ya kuijenga, tayari upembuzi yakinifu, tathmini ya athari kwa jamii na mazingira, usanifu, makabrasha ya zabuni na kilometa 14.4 zimeshajengwa kama hatua ya awali.
pale na akimaliza muda wake Rais ajaye ataendelea na utkelezaji.

0 comments:

Post a Comment