
Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
“Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani
walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80 (wa kishindo), huu ulikuwa ushindi
wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni
kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia hususan ushindani wa
vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika.
Kauli hiyo ya Makamba imekuja wakati matokeo ya
serikali za mitaa yakionyesha kuwa CCM imeporomoka kutoka ushindi wa
asilimia 91.7 mwaka 2009 hadi 79.8 katika uchaguzi wa mwaka jana na
upinzani ukipanda kutoka asilimia nane mwaka 2009 hadi takriban 20 mwaka
jana.
Akizungumza jana katika mahojiano na kipindi cha
‘Power Breakfast’ cha Redio ya Clouds na baadaye kufafanua baadhi ya
hoja alipozungumza na mwandishi wetu, Makamba alisema matokeo ya
uchaguzi huo ni ishara kwamba kwa umri wa miaka 22 sasa, mfumo wa vyama
vingi vya siasa umeanza kuimarika.
“Hata ushindi wa asilimia 81 tulioupata katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni mkubwa na hata kama tungepata asilimia 70 haupunguzi uhalali wa uongozi. Kusema CCM itang’oka madarakani, hapana, bado wananchi wanakiamini tena sana,” alisema Makamba.
Makamba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, alizungumzia pia namna ya kuwapata wagombea wa urais na
kusema mwaka huu ndiyo utapima ukomavu wa chama katika harakati za
kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete.
Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa London,
Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema mwaka
1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere, mwaka
2000 aliendelea aliyekuwa
Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa London, Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema mwaka 1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 2000 aliendelea aliyekuwapo.po. Alisema mwaka 2005 ilikuwa kama 1995 lakini mwaka huu ni tofauti na vipindi vingine kabisa.
Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa London, Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema mwaka 1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 2000 aliendelea aliyekuwapo.po. Alisema mwaka 2005 ilikuwa kama 1995 lakini mwaka huu ni tofauti na vipindi vingine kabisa.
“Hii ni mara ya kwanza hakuna uhakika wa nini
kitatokea na kwa mara ya kwanza chama chetu kama taasisi kitajaribiwa...
na sisi tuna utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa.
“Tuna sifa 13 za kumpata mgombea, sifa hizi na
taratibu nyingine zikifuatwa tutampata. Mchakato ukiwa wa haki tutampata
kwani nina imani na mwenyekiti (Rais Kikwete), Katibu Mkuu (Abdulrahman
Kinana) na Kamati Kuu,” alisema Makamba .
Ujana na uzee
Kuhusu hoja ya ujana au uzee ambayo imewagawa
wagombea urais wa CCM, Makamba alisema kuna tofauti kati ya umri, uwezo
na uzoefu ili wananchi waweze kumwamini mtu na kumpa fursa ya
kuwatumikia, jambo ambalo alisema halihitaji kutumia fedha nyingi au
kuweka mbele uchu wa madaraka ili kuyafanya mazingira yawe ya lazima
kupata.
“Nchi ipo njiapanda na mwaka huu ndiyo itaamua
kupaa au kuporomoka lakini kumchangua kiongozi ambaye ameshiriki kuuweka
mfumo huu wa uongozi unaolalamikiwa sasa ni kurudisha nyuma maendeleo.
Kuna vijana viongozi na viongozi vijana. Kuna vijana ambao wameandaliwa
vyema kuja kushika uongozi wa juu, hivyo tukipata viongozi wa sasa
wanaojua ulimwengu wa sasa, nchi yetu itaweza kupaa zaidi,” alisema
Makamba.
Kuhusu uzoefu
Akizungumzia uzoefu wa uongozi hasa urais, Makamba
alisema Tanzania ina watu wanne pekee, mmoja akiwa marehemu, ambao
ndiyo wazoefu na uongozi wa juu ambao ni Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Nyerere, marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na Rais
Kikwete anayemaliza muda wake.
“Hakuna yeyote tofauti na hawa wanne anayeweza
kusema ni mzoefu... Vijana wanaweza lakini tusingependa kurudi katika
hoja hii na kinachotakiwa ni kubadili taswira ya uongozi kabisa ni
wakati wa fikra na mawazo mapya.
“Kuna watu wamekuwa viongozi kwa zaidi ya miaka 40
lakini leo hii hawataki Muungano na kuna vijana ambao wanautaka hivyo
hapa hoja siyo umri au uzoefu, bali ni kipi ambacho unataka kukifanya
katika Taifa lenye kila aina ya rasilimali,” alisema Makamba, mtoto wa
katibu mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba.
Akizungumzia kitabu alichoandikiwa kinachoitwa,
Maswali na Majibu 40: Mazungumzo na January Makamba kuhusu Tanzania Mpya
alisema wananchi wanatakiwa kumjua kiongozi wanayetaka kumpa dhamana
hivyo andiko hilo linatakiwa kuzua mjadala.
“Taifa litasonga mbele kama wananchi watamchagua
kiongozi ambaye wanamfahamu, tusiwe kama msemo unaosema tusiuziwe mbuzi
kwenye gunia,” alisema.
Akijibu swali la na mmoja wa watangazaji wa
kipindi hicho, aliyetaka kujua kama malengo yake aliyobainisha katika
kitabu hicho yatafanikiwa kutokana na Watanzania wengi kutokuwa na
utamaduni wa kujisomea alisema: “Sifa ya Mwalimu Nyerere alikuwa na
dhana ya kuandika maandiko lakini si kweli kwamba Watanzania hawasomi,
hapana, ukiangalia hata magazeti sasa yameongezeka, wangekuwa hawasomi
yangekuwa magazeti mawili tu. Ila wanasoma mambo yanayowahusu na tumeona
kitabu hiki kilivyopokewa sikutarajia na wengine sasa waandike maandiko
ili wananchi waweze kuwafahamu.”
Kuhusu uhusiano wake na Rais Mwinyi kutokana na
kuandika dibaji katika kitabu hicho na iwapo anamuunga mkono katika
harakati zake za urais, Makamba alijibu, “Hapana na nisingependa
kuzungumza kwa niaba yake na yeye kukubali kuandika dibaji kuwa yuko
nyuma yangu, siyo kweli na nisingependa kumwingiza katika siasa zetu
lakini maelezo yake yanaeleweka... tusipende kumkwaza.”
Katika dibaji ya kitabu hicho, Mzee Mwinyi alisema
Makamba anaonekana dhahiri ameandaliwa au amejiandaa vilivyo kuwa
kiongozi mkubwa wa nchi.
Mzee Mwinyi anasema kitabu hicho kimemfanya
amfahamu zaidi kiongozi huyo kuliko awali alipokuwa kama kiongozi ndani
ya chama na Serikali.
Anaeleza kufarijika kwake kuona nchi na Rais
Kikwete wameendeleza utamaduni aliouanzisha Mwalimu Nyerere na
kuendelezwa naye wa kuwaamini vijana na kuwapatia fursa za uongozi ili
kuwaandaa kuongoza nchi.
0 comments:
Post a Comment