Pages

Subscribe:

Tuesday 27 January 2015

CHANZO CHA BIFU LA ALI KIBA NA DIAMOND HIKI HAPA!!...Soma zaidi upate undani




Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
KWENU wakali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba. Bila shaka mko poa na mnaendelea na mishemishe zenu za kila siku.
Mkitaka kujua hali yangu, mimi ni mzima wa afya na ninaendelea na majukumu yangu ya kila siku kuhakikisha mkono unaenda kinywani kama nyinyi mnavyofanya muziki kujitengenezea mamilioni.
Madhumuni ya kuwakumbuka leo kupitia barua hii ni kutaka kuwaonya juu ya vitendo vya kuzomeana maarufu kama buuu. Kinachonisikitisha ni kwamba nyinyi wenyewe ndiyo mnatajwa katika kusuka mipango ya kuzomeana.
Mnatajwa kuwa mnawalipa vijana vijisenti ili waweze kuharibu shoo. Hivi mnafikiri katika hili mnakomoana au mnajiharibia wenyewe? Juzikati kwenye shoo yenu iliyowakutanisha pale kwenye Viwanja vya Leaders Club kamchezo hako kalitokea.

Mbaya zaidi kalishajulikana katatokea kabla hata ya shoo hiyo kufanyika. Hii inaonesha ni jinsi gani mnajiandaa kufanya jambo la kuharibiana.
Hivi vitu mnavilea. Vinakua na madhara yake ni makubwa. Wale watu waliokuwa wanamrushia chupa Diamond akiwa jukwaani, wangempasua uso ingekuwaje?
Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba.
Katika hili wala hakuna haja ya kumtafuta mchawi. Mnajiroga wenyewe sababu mmekuwa wazito kuonesha dhahiri kwamba hamna tatizo kati yenu. Machoni kwa wengi au mkihojiwa katika vyombo vya habari mnasema hamna tofauti kumbe moyoni hampendani.
Hii siyo sawa. Matendo yenu ndiyo yanayodhihirisha kwamba hampo sawa bali mnajaribu kuficha makucha, mnaweza kufanya vita hii ya chinichini halafu likaja kutokea jambo kubwa katika majukwaa ambalo pengine mngechukua tahadhari wala lisingetokea.
Kwanza mnawagawa mashabiki. Wapo ambao wakiona mnaendeleza chuki watawaacha na kushabikia wasanii wengine.
Nyinyi mnapaswa kuwaamisha mashabiki kwamba hamna tofauti. Mnapaswa kuzunguka pamoja na kuonesha kwa vitendo kwamba hamna tofauti.
Mshindane kuimba lakini msihamishie mashindano katika kuandaa vikundi hivyo ambavyo mnavinunua ili vifanye fujo.
Kama msanii imba muziki mzuri mashabiki watakupa sapoti. Hakuna haja kuwekeana chuki zisizokuwa na maana. Tena kama hamjui, huu ndiyo muda wa kufanya ‘idea’ ya shoo ya pamoja.
Andaeni shoo moja ambayo inaweza kuwaaminisha mashabiki kwamba hamna tofauti. Chuki zikizidi mnaweza kuuana hivihivi. Mashabiki wanachochewa na nyinyi.
Nyinyi mkimaliza tofauti zenu hata wao hawawezi kuendelea kuzomea wala kurusha chupa hizo majukwaani.
Kila mmoja afanye muziki wake, wote muwe na azimio moja tu, kuufikisha muziki wa Bongo Fleva katika levo za kimataifa.

0 comments:

Post a Comment