Pages

Subscribe:

Wednesday 21 January 2015

Marais watano kushuhudia amani Sudan Kusini



Marais watano wa nchi za Afrika, leo watashuhudia utiaji saini wa mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini, yatakayofanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Marais hao ni Jacob Zuma (Afrika Kusini), Yoweri Museveni (Uganda), Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini), mwenyeji wao Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn Boshe.


Mazungumzo hayo yanayoratibiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), yalianza Oktoba 12, 2014 na kuwahusisha viongozi wa chama tawala cha Sudan People Liberation Movement (SPLM) ambao wamegawanyika.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete juzi alituma timu ya wajumbe wa mazungumzo hayo kwenda Uganda na Sudan Kusini kuonana na viongozi wa makundi yanayopingana.
Timu ya ujumbe huo, inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ilitarajiwa jana jioni kuwasilisha taarifa kwa Rais Kikwete.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Filex Ntibenda alithibitisha kuwapo kwa maandalizi ya mkutano huo na kudai hajapata ratiba.

0 comments:

Post a Comment