Niaje…niaje
masela wangu? Kitaa hiyo kwa fasi ya kati barida? Mitikasi vipi wana?
Kama freshi basi ndo mpango mzima! Ama nini? Basi mzuka kwa wingi
chaliiangu.
Karibu jamvini mazee nikusanue ishu bee za kitaa. Machalii hivi laifu mnalionaje kwa saidi yenu? Kipande hii ni fulu mastresi na bado sisomeki aisee arifu.
Karibu jamvini mazee nikusanue ishu bee za kitaa. Machalii hivi laifu mnalionaje kwa saidi yenu? Kipande hii ni fulu mastresi na bado sisomeki aisee arifu.
Tudei
bana nitakugonga na limkasa la mwanangu Jeff. Ni kitambo kiduchu
kimekrosi. Unajua nini kilihapeni?Mwanangu alizima fegi kwa mtoto mmoko
mkare aibu. Yaani mbebiz wa ukwehe kabisa. Si unajua zile za umbo namba
nane dheni rangi ya chokleti? Selaa anakuteli kuwa mtoto ni smati
kichwani. Sasa ukiwa na shori kama huyo laifu linataka nini tena? Kaa
humu wewe upate kitu roho inataka.
asi
mtu mzima, kaka mkubwa mwenyewe, akaona ngoja ajaye kwenye kumi na nane
za shori. Jamaa akajitoa kitu cha fahamu akaona amepata waifu wa
kuspendi naye.Kweli bana, mtoto akajifanya kumwelewa mwana na laifu
likasonga fasta kinomanoma. Huku na huku shori akaanza kufosi kitu cha
mereji kama ilivyo kwa makiksi wengi wa tauni nawu deizi. Siku hizi ndo
zao. Ukijichanganya tu imekula kipande yako na ukitaka kung’oa kirahisi
wewe mpromisi mereji.
Diferenti
na mbebizi mkare, mwanangu yeye hakuwa na mudi kozi aliona bado taimu
ipoipo so hamaindi ishu za kiloko za kuharakisha au kukurupuka. Wazazi
asikumiksi mtu maana hutachukua raundi, utaanza kuzinguliwa dheni aibu
mazee.
Msela
anaamplifai kwamba alipomuwekea ngumu na kumfungukia ukweli kuwa bado
yupoyupo sana, mtoto mkare akamaindi kinoma. Jamaa akaona isiwe kitu,
akamwaambia anaweza kupita hivi yaani kujivua gamba.
Kweli
shori aliuchubua kama wiki bee hivi. Kachaa wangu kitu cha moyo
kilimuuma hatari kozi alikuwa amezimika ileile kwa mtoto mzuri.Baada ya
wiki bee, uzalendo ukamshinda shori. Akarejesha majeshi dheni akajaribu
kumpliizi mwanangu kuwa waendelee na malovee na kwamba alikuwa yupo rede
kutumika ipasavyo. Sasa kidume upewe promisi ya aina hiyo na shori
mzuri utauliza cha kufanya? Watoto wa mbwa wanakuteli kuwa ushindwe
mwenyewe kujilia vyako.
Kweli
jamaa aliinjoi mavitu bati leita alishtuka kuwa shori alikuwa na mpango
wa kando na jamaa aliyeingia kingi kumpiga kitu cha pingu za
maisha.Msela wangu akaona isiwe kitu akamwachia shori akaenda zake
kulianzisha na jamaa’ke aliyekuwa akishea naye mambo f’lani. Ebana
hakuna soo baya kama kushtukia kuwa shori wako unashea na msela.
Kuliko kushea shori, beta ukauteli moyo uvumilie maumivu bati utemane naye.
Basi bana, shori si akaangushiwa bonge la sendi ofu dheni kitu cha mereji. Kweli watu waligonga mnuso bati tunaposebenza hapa mtoto mkare yupo mahomu kwao ameshamwagwa.
Basi bana, shori si akaangushiwa bonge la sendi ofu dheni kitu cha mereji. Kweli watu waligonga mnuso bati tunaposebenza hapa mtoto mkare yupo mahomu kwao ameshamwagwa.
Unajua kilichohapeni?
Mdada anataka kurudi kwa msela wangu kozi ameshamuibukia analia kinoma mazee.
So
msela wangu yupo njiapanda amkubalie au amwache atambae? Ungekuwa wewe
ungefanyaje wakati inaeleweka kabisa kwamba huwezi kuosha mkaa ili
utakate.
Masela tafakarini dheni mchukue hatua. Mmenisoma?
Kama vipi kitu cha wikiendi kwa mbaliii…sii yuu neksti wiki.
Masela tafakarini dheni mchukue hatua. Mmenisoma?
Kama vipi kitu cha wikiendi kwa mbaliii…sii yuu neksti wiki.
0 comments:
Post a Comment