UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firahuni! Binti aliyefahamika kwa jina moja la Afsa (14), anayesoma darasa la 7, ametiwa nguvuni na jeshi la polisi akidaiwa kuwafanyia ukatili na kuwadhalilisha watoto wawili wa kiume (majina kapuni) wa mama yake mkubwa kwa kuwakang’ata nyeti zao akiwalazimisha kufanya nao mapenzi.
Tukio hilo la kushangaza ambalo lilijaza
umati wa watu , lilitokea wiki iliyopita katika mtaa wa Nyerere, Kata ya
Mafisa, mkoani hapa.
Kamanda wa OFM, Mkoa wa Morogoro akiwa kazini, alipokea taarifa kutoka kwa wananchi wa mtaa huo wakimuomba afike fasta.
Bila kuchelewa kamanda alitia timu na kukutana na akina mama wawili ambao walishusha ‘vesi’ za tukio hilo:
Kamanda wa OFM, Mkoa wa Morogoro akiwa kazini, alipokea taarifa kutoka kwa wananchi wa mtaa huo wakimuomba afike fasta.
Bila kuchelewa kamanda alitia timu na kukutana na akina mama wawili ambao walishusha ‘vesi’ za tukio hilo:
“Sisi ni wakazi wa mtaa huu wa Nyerere ambao tunaishi na Mama Mese mwenye watoto wawili wa kiume, anaishi pia na mtoto wa mdogo wake (Afsa) aliyempa jukumu la kuwalea wanaye.
“Cha kushangaza Afsa amekuwa akiwafanyia ukaliti wa kutisha watoto hao. Leo amewatoboa macho na njiti ya viberiti kuwapiga mateke na kuwasukumiza ukutani, mbaya zaidi aliwang’ata nyeti zao alipokuwa akiwalazimisha kuduu nao.
Mwanahabari wetu alifika kwenye nyumba hiyo
na kumkuta mama Mese akiwa na watoto wake hao wakiwa na makovu mwili
mzima, alipoulizwa undani wa tukio hilo na kwa nini hatoi taarifa katika
vyombo vya usalama? Alifunguka:
“Mimi ni mfanyakazi pia mwanafunzi, nasoma chuo hivyo wanangu
hulelewa na Afsa ambaye ni mtoto wa mdogo wangu. Kweli wanangu wamepigwa
na kufanyiwa ukatili na huyu mtoto wa mdogo wangu lakini suala hili
sitaki lifike popote, nimepanga kumrudisha kwao Moshi,” alisema Mama
Mese.Katika hali ya kushanga, paparazi wetu alipotaka kumhojia Afsa, mama huyo alikataa jambo lililowakera majirani na kuibua vurugu.
Baada ya vurugu kuwa kubwa, jirani mmoja aliwatonya polisi ambao walifika ndani ya muda mfupi na kufanikiwa kumkamata Afsa kumpeleka kituoni kwa ajili ya hatua za kisheria huku mjumbe wa serikali ya mtaa
huo, Yusuf Juma akishuhudia tukio hilo na kulilaani.
0 comments:
Post a Comment