Miss Colombia, Paulina Vega baada ya kuvishwa taji la Miss Universe 2015.



MISS Colombia, Paulina Vega atwaa taji la Miss Universe 2015 katika
fainali zilizofanyika jana huko Miami nchini Marekani huku umati
ukizomea kuonyesha kutoridhika na matokeo hayo.
Umati uliohudhuria fainali hizo ulitarajia Miss Jamaica Kaci Fennell aliyeshika nafasi ya
nne kutwaa taji hilo lakini ulionyesha kushangazwa na maamuzi ya majaji kumtangaza Miss Colombia Paulina Vega mwenye miaka 22.
Zomea zomea zilisikika mara baada ya mshindi huyo kutangazwa huku kukiwa na minong'ono ya hujuma katika mashindani ya mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment