
MSANII nyota wa Bongo Fleva Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz,’ na mshindi wa shindano la Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan, juzikati waliwaliza machozi ya furaha walimu wao wa shule ya Mbezi High School iliyopo Kimara walikosoma, baada ya kufika ghafla kwa ajili ya kuwasalimia.
...Wakiongea na wanafunzi wa shule hiyo.
“Tuliamua kwenda shuleni baada ya kugundua kuwa wote tulisoma pale,
nilikutana na walimu walionifundisha pamoja na baadhi ya wafanyakazi,
hii ilitufariji sana. Tumekubaliana kwamba wakati wa mahafali yao
tutakuwa tukifika ili kuwapa sapoti kama wakati huo tutakuwa tupo hapa
mjini,” alisema Dimpoz, ambaye anafanya vizuri katika muziki huo wa
kizazi kipya.
0 comments:
Post a Comment