Walitoa ombi hilo jana kwenye kikao cha Bodi ya
Barabara ya Mkoa wa Iringa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Siasa ni
Kilimo, Manispaa ya Iringa.
Wadau hao waliamua kuunda timu maalumu itakayokutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda au Rais Kikwete kwa ajili ya kuwasilisha ombi maalumu la kuharakisha ujenzi huo. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Steven Mhapa alisema ubovu wa barabara hiyo umeendelea kuzorotesha sekta ya utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamudu
Mgimwa alisema Mkoa wa Iringa unapaswa kuwa na mkakati wa kuzipigia
debe barabara zote zinazobeba uchumi wa nchi kama ilivyo kwa barabara
hiyo ya Hifadhi ya Ruaha.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Profesa Peter Msolla
alisema mbali na kuikuza sekta ya utalii mkoani Iringa, kujengwa kwa
kiwango cha lami kwa barabara hiyo kutachochea uanzishwaji wa shughuli
mbalimbali za kiuchumi zenye uhusiano na sekta hiyo na hivyo kusaidia
kuongeza ajira hususani kwa vijana.
Awali, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania
(Tanroads) Mkoa wa Iringa, Paul Lyakurwa alisema baada ya Rais Kikwete
kutoa ahadi ya kuijenga, tayari upembuzi yakinifu, tathmini ya athari
kwa jamii na mazingira, usanifu, makabrasha ya zabuni na kilometa 14.4
zimeshajengwa kama hatua ya awali.
pale na akimaliza muda wake Rais ajaye ataendelea na utkelezaji.
0 comments:
Post a Comment