
Thursday, 29 January 2015
Wednesday, 28 January 2015
Tuesday, 27 January 2015
HIZI NDO PICHA MPYA ZA KIMAHABA ZA MAUNDA ZORRO!! NI NOOOOMAAAA!!!
Maunda Zorro Kwenye Pozi la Kimitego |
Friday, 23 January 2015
Wednesday, 21 January 2015
HII NDO AINA YA USALITI USIOVUMILIKA!!


Anasemaje? Hebu msikie kwanza kisha tuendelee; “Mimi na mume wangu tulikuwa tunapendana sana na hajawahi kunisaliti. Tulioana miaka mitatu iliyopita na sasa nina ujauzito wa miezi nane.
“Mume wangu anafanya kazi na mimi pia nafanya kazi lakini kipato changu ni kikubwa kumzidi mume wangu.
“Kutokana na hali hiyo, mimi nilinunua gari ambalo mume wangu amekuwa akilitumia muda mwingi. Huwa ananipeleka kazini kisha yeye anaenda kwenye mihangaiko yake, jioni ananifuata. “Tunaishi na mdogo wangu wa kike ambaye anasoma chuo ila alionesha ukaribu sana kwa mume wangu, utani ulikuwa mwingi hadi kuna kipindi nikahisi kuna kitu nyuma ya pazia.
“Siku moja baada ya mume wangu kunipeleka kazini, tulimuacha nyumbani yule mdogo wangu, ilikuwa aende chuo lakini nikashangaa siku hiyo akasema hataenda. “Machale yakanicheza! Baada ya mume wangu kunifikisha kazini na kuondoka, nikakaa kama nusu saa hivi kisha nikachukua Bajaj na kurudi nyumbani.
“Huwezi kuamini nilimkuta mdogo wangu akifanya mapenzi na mume wangu juu ya kitanda changu. Nilipata presha na kuanguka, nilipozinduka nilijikuta nikiwa hospitalini.“Mpaka sasa niko kwa wazazi wangu na nakaribia kujifungua. Hivi kwa usaliti huu naweza kumsamehe mume wangu na tukaishi kwa amani?”
Huo ni ushuhuda wa Ashura ambaye mwisho wa siku aliomba nimshauri. Ingekuwa wewe ungemshaurije? Je, ungemshauri arudi kwa mumewe au ungemtaka aombe talaka?
Najua kwa vyovyote ungekuwa na la kumshauri lakini mimi ninavyoona kwa hili ni lazima uwe njia panda. Yaani mdogo wako umkute kamvulia nguo mumeo na wanafanya uzinzi juu ya kitanda chako! Ukisikia watu wanaua ni katika mazingira haya.

Wapo ambao wamewafumania wanandoa wenzao mara kibao lakini mpaka leo bado wanaishi pamoja na wanasimamia ule msemo usemao; ‘Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo’.Lakini wakati hao wakiwa na mioyo hiyo, kuna ambao wameachana baada ya mmoja kukuta tu sms tata kwenye simu ya mwenza wake.
Kwa hili la Ashura iko hivi, hakuna usaliti usiouma, uwe ni mdogo au mkubwa. Usaliti aliofanyiwa Ashura ni mkubwa sana, huwezi kumshauri kirahisi tu kwamba amsamehe mume wake na arudi kwake.Lakini pia huwezi kumshauri kwamba kwa kuwa ni usaliti mkubwa basi asimsamehe na aombe talaka.
Ushauri wote unaweza kuwa sawa lakini pia unaweza usiwe sawa. Kutokana na mazingira, kwamba Ashura ni mjamzito na mume wake hajawahi kumsaliti, kuna kila sababu ya kusamehe.Kama mume ameomba msamaha na kuahidi kubadilika, kumgomea itakuwa ni vigumu.
Lakini naomba niseme kwamba, kwenye suala la usaliti ni vyema tukazungumza na mioyo yetu. Ukijaribu kufuatilia utabaini hakuna ambaye hajawahi kusalitiwa na mpenzi wake. Tunachokifanya huwa ni kusamehe na kusahau hasa tukichukulia kwamba, wote tuna mapungufu. Ni kweli kuna usaliti usiovumilika, kwa mfano kama amekuwa akikusaliti kila wakati, huyo ifike wakati useme imetosha.
Lakini kama unampenda na kwa bahati mbaya akawa amekusaliti kwa mara ya kwanza, ni vyema ukampa nafasi nyingine bila kujali watu watasemaje. Kwa maana hiyo licha ya kwamba usaliti si mzuri lakini usichukue uamuzi wa kumuacha mwenza wako au mpenzi wako kwa sababu ya usaliti wa mara ya kwanza, ukifanya hivyo ipo siku utajuta.
Makamba: Enzi za ushindi wa kishindo CCM zimepita

Marais watano kushuhudia amani Sudan Kusini
Marais watano wa nchi za Afrika, leo watashuhudia utiaji saini wa mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini, yatakayofanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Marais hao ni Jacob Zuma (Afrika Kusini), Yoweri
Museveni (Uganda), Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini),
mwenyeji wao Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Desalegn Boshe.
Mapya yaibuka kuapishwa kwa mwenyekiti wa Segerea-Migombani

Wakili wa Kujitegeme, Iddi Msawanga(kulia) akimuapisha Japhet Kembo (aliyenyanyua mkono) kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Migombani, katika hafla iliyofanyika nje ya ofisi za mwenyekiti wa mtaa huo, Segerea Mwisho Dar es Salaam . Japhet aligombea nafasi hiyo kupitia chama cha Chadema
Anna Abdallah ataka vigogo wapigwe rungu

Kauli ya Mwakyembe yaamsha wadau
Shirika la Ndege la Flight Link la Dar es Salaam limesema litaanza kutoa huduma ya usafiri wa anga kati ya Dar es Salaam na Iringa muda wowote kuanzia sasa.
Uamuzi wa Flight Link kuanzisha huduma hiyo,
umekuja siku chache baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
kufanya ziara mkoani hapa na kushawishi wadau wa usafiri wa anga kutoa
huduma mkoani hapo.
mwanzo Kolamu Kolamu Fidel Castro; mtoto wa ‘housegirl’ aliyekabili vigingi vingi kwenda Ikulu- 2
Wiki iliyopita tuliona Fidel Castro alikwama
kwenye ndoto yake ya kugombea ubunge baada ya mapinduzi ya kijeshi
yaliyoongozwa na Generali Fulgencio Batista na kuvuruga demokrasia.
Castro hakukubaliana na
mapinduzi hayo na alikuwa miongoni mwa walioupinga utawala wa Batista na
mara kadhaaa alijaribu kutumia sheria pasipo mafanikio.
Monday, 19 January 2015
Wahoji utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete
Wadau wa maendeleo mkoani Iringa, wameitaka Serikali itekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kutengeneza Barabara ya Iringa-Msembe (Hifadhi ya Taifa ya Ruaha) yenye urefu wa kilomita 114 kwa kiwango cha lami ikiwa ni jitihada za kukuza uchumi wa mikoa ya Kusini.
Walitoa ombi hilo jana kwenye kikao cha Bodi ya
Barabara ya Mkoa wa Iringa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Siasa ni
Kilimo, Manispaa ya Iringa.
Wahoji utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete
Wadau wa maendeleo mkoani Iringa, wameitaka Serikali itekeleza
ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kutengeneza Barabara ya Iringa-Msembe
(Hifadhi ya Taifa ya Ruaha) yenye urefu wa kilomita 114 kwa kiwango cha
lami ikiwa ni jitihada za kukuza uchumi wa mikoa ya Kusini.
Walitoa ombi hilo jana kwenye kikao cha Bodi ya
Barabara ya Mkoa wa Iringa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Siasa ni
Kilimo, Manispaa ya Iringa.
Wanafunzi 150 Duce wapata mimba
Wanafunzi 150 kati ya 1,000 waliojiunga na masomo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce) mwaka jana wamebainika kuwa na ujauzito waliopewa na wenzao chuoni hapo.
Utafiti wa usawa na jinsia uliofanywa na chuo
hicho kati ya Juni na Novemba mwaka jana umebaini kuwa wanafunzi
wanaopata ujauzito ni wale wa mwaka wa kwanza.
Subscribe to:
Posts (Atom)