ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa maafande wa JKT Ruvu, Salum Machaku, amesema mpaka sasa hajapata timu na yupo tayari kujiunga na timu yoyote kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao.
Machaku aliyewahi kuitumikia Klabu ya Simba kwa mafanikio kipindi cha nyuma, amemaliza mkataba wake na maafande hao.
Mchezaji huyo mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, baada ya kumaliza mkataba na JKT, Simba iliwahi kumtaka lakini anashangaa mpaka sasa wapo kimya, hivyo timu yoyote itakayovutiwa kufanya naye kazi, yupo tayari kuingia mzigoni muda wowote kuanzia sasa.
“Kwa sasa nafanya mazoezi binafsi kwenye viwanja tofauti kwa lengo la kujiweka sawa kwa msimu ujao.
“Simba walikuwa wakinihitaji, lakini naona kimya sana, sasa kama kuna timu yoyote inahitaji huduma yangu ije tuzungumze, kikubwa ni maslahi tu, soka ndiyo kazi yangu,” alisema Machaku.
0 comments:
Post a Comment