Pages

Subscribe:

Wednesday 16 July 2014

WEMA, PENNY WAKAA MEZA MOJA KUMJADILI DIAMOND!!



Staa wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu
amesema baada ya kutokuwa na
maelewano kwa muda mrefu na mtangazaji
maarufu Bongo, Peniel Mungilwa 'Penny',
sasa ameamua kumsamehe rasmi kwa
heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko,
Wema alisema: "Kwa moyo mweupe,
nasema nimemsamehe Penny, hata
nikikutana naye popote nitasalimiana naye
kama kawaida. Nimeamua kuachana na
yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji
sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa
Mungu."

Kwa upande wa Penny alifunguka: "Siwezi
kusema nitamchukia Wema ila nimekubali
matokeo, sina tatizo naye tena ingawa
najua hatuwezi kuwa marafiki tena kama
zamani, lakini yaliyopita yameshapita."
Wema na Penny walikuwa na bifu kwa
muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia
uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo
Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond'.
Credit: Risasi Mchanganyiko

0 comments:

Post a Comment