Pages

Subscribe:

Wednesday 23 July 2014

RAY, CHIKI NUSURA WAZICHAPE!




ILIBAKI kidogo mastaa wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, na Salum Mchoma ‘Chiki’, wazichape baada ya kutokea mzozo kati yao uliodumu kwa dakika tatu wakirushiana maneno.
Staa wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Tifu hilo lilitokea wikiendi iliyopita, Lamada Hotel – Ilala, Dar ambapo Chiki alimshukia Ray akidai kuwa (Ray) haungi mkono uongozi wa Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ ndiyo maana alikacha sherehe yake hivi karibuni.
Maneno ya Chiki yalimchoma Ray ambaye alionekana dhahiri kupaniki lakini akajibu mapigo: “Siwezi kuacha kazi location ili niwahi sherehe, huo ndiyo utaratibu wangu, hata hapa (kwenye birthday ya Dk. Cheni) nimekuja kwa sababu sina kazi yoyote inayoendelea.
Staa wa sinema za Kibongo, Salum Mchoma ‘Chiki’
“Siwezi na sina sababu ya kumpinga Steve Nyerere, sikwenda kwenye shughuli yake kwa sababu nilikuwa narekodi... filamu ndiyo maisha yangu, acha kuropoka wewe.”

0 comments:

Post a Comment