Pages

Subscribe:

Monday 21 July 2014

TAARIFA JUU YA WAUMINI 30 WA KANISA LA MORAVIAN KUFIKISHWA KORTINI KWA KUFANYA VURUGU

Hii ni safari ya kwenda kusomewa mashitaka yao.

Akina mama wakificha sura zao baada ya kutoka mahakamani.
Watuhumiwa wakiingizwa mahakamani.  Wakitoka kusomewa mashitaka.  Wakili Henzron Mwakenja akipokea hati ya dhamana kwa watuhumiwa.
Waumini wa kanisa la Moravian wakificha sura zao wakati wa kuingia mahakamani.

Kundi la kwanza la waumini waliokuwa wanasali nje
Hili ndilo kundi la pili la waumini waliokuwa wanasali ndani.
Askari wakiwa eneo la mahakamani.
Baadhi ya ndugu na waumini wa Moravian wakiwa nje ya geti la mahakama.
Majina na nyaraka ya watuhumiwa wa  vurugu za kanisa la Moravian.
Kesi namba inayowakabili waumini hao.


WAUMINI wapatao 30 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hadharani katika Kanisa la Moravian lililopo Mwananyamala-Msisiri ” A” Wilaya ya Kionondoni.
Katika kesi hiyo iliyounguruma kwa muda wa saa mbilli imeelezwa kuwa Julai 20 mwaka  huu katika  kanisa hilo lililopo eneo la Mwananyamala Msisiri ‘A’ waumini  hao kwa  pamoja walifanya  fujo  zilizosababisha kuhatarisha amani.
Kesi hiyo iliyosomwa na mwendesha mashitaka wa serikali, Credo Rugajo mbele hakimu mwandamizi  wa  mahakama hiyo Boniphace Lihamwike, ilidaiwa kuwa Julai 20 waumini walianzisha mzozo uliosababisha waumini kupigana  na kusababaisha askari  polisi  kutumia  nguvu  kubwa  kutuliza  fujo  hizo  ikiwa ni pamoja na kutumia mabomu ya machozi.
Baada ya  kusikiliza kesi pande zote  mbili, Hakimu Lihamwike alisema dhamana iko wazi  kwa  kila  mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika na shilingi  milioni moja  kimaandishi kwa  kila  mmoja.
Kesi  hiyo imeahirishwa hadi  Agosti 4 mwaka huu itakaposikilkizwa  katika mahakama hiyo

0 comments:

Post a Comment