
KERO! Mtendea haki sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa anakerwa sana na wanaume wenye hulka za kike (mashoga).
Akichonga na paparazi wetu, Aunt alisema mashoga wanamstaajabisha kwa jinsi wanavyojiweka na kujishaua katika jamii kitu ambacho anaamini ni tabia mbaya ambayo mtu anaweza kuiacha mara moja.
“Mashoga hunistaajabisha sana kwa kweli, kila niwaonapo sijui najisikiaje? Nawashangaa kweli, kwa nini wasibadilike,” alisema Aunt.
0 comments:
Post a Comment