Pages

Subscribe:

Monday 21 July 2014

BRAZIL 2014: Rekodi nyingi zavunjwa

Hivi sasa tunasubiri miaka mingine minne ijayo kwa ajili ya kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia 2018. Hata hivyo ni vizuri tukiziangalia kwa mtindo wa namba Fainali za Kombe la Dunia 2014 zilizomalizika wiki iliyopita:

0: Ni namba ya wachezaji wa Ligi Kuu England katika kikosi cha Fainali za Kombe la Dunia 2014 kilichochaguliwa baada ya kumalizika fainali hizo.

1: Bao moja lililofungwa na Mario Gotze katika mechi ya fainali lilitosha kuipa Ujerumani ubingwa wa dunia 2014.

1: Kipa wa England, Joe Hart aliokoa mara moja mpira wa hatari katika mechi mbili za Kombe la Dunia huku akikubali kufungwa mabao manne.

2: Thomas Muller (2010 & 2014) na Miroslav Klose (2002 & 2006) ni wachezaji pekee ambao wamefunga mabao matano katika Fainali za Kombe la Dunia mbili tofauti.

3: Ni idadi ya mashuti ya mchezaji bora wa Fainali za Kombe la Dunia 2014 yaliyolenga lango katika mechi nne za hatua ya mtoano.

5: Hispania ilikubali kuruhusu mabao matano katika mechi moja (5-1 dhidi ya Holland) kwa mara ya kwanza tangu ilipofungwa 6-2 na Scotland Juni 1963.

6: Mshambuliaji wa Ghana, Asamoah Gyan alifikisha mabao sita katika Fainali za Kombe la Dunia 2014 na hivyo kuvunja rekodi ya Roger Milla ya mabao matano ya kuongoza kufunga kwa wachezaji wa Afrika katika Kombe la Dunia.

6: Ni timu sita tu za Ulaya ambazo zimefika hatua ya 16 bora katika Fainali za Kombe la Dunia 2014; kiwango hicho ni cha chini kwa timu za Ulaya tangua hatua ya 16 bora ilipoanzisha 1986.

7: Ni dakika ambazo Argentina imekuwa nyuma katika mashindano hayo. Dakika hizo zilikuwa katika mechi ya fainali dhidi ya Ujerumani baada ya kufungwa bao 1-0 na Ujerumani katika dakika 113.

7: Ushindi wa Ujerumani wa mabao 7-1 dhidi ya Brazil ndiyo ushindi mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika nusu fainali ya Fainali za Kombe la Dunia.

8: Ni idadi ya mechi ambazo zilichezwa kwa muda wa nyingeza wa dakika 30, idadi hiyo ya mechi pia ilipatikana katika Fainali za Kombe la Dunia za 1990 zilizofanyika Italia.

10: Ni idadi ya kadi nyekundu walizopewa wachezaji katika Fainali za Kombe la Dunia 2014.

10: Sami Khedira ni mchezaji wa 10 kutwaa ubingwa wa Ulaya na ubingwa wa dunia katika msimu mmoja.

12: Ni idadi ya penalti zilizofungwa katika Fainali za Kombe la Dunia 2014 ndani ya muda wa mechi.

12: Ni idadi ya makocha waliojiuzulu baada ya kumalizika Fainali za Kombe la Dunia 2014.

15: Kipa wa Marekani, Tim Howard aliokoa michomo 15 katika mechi ya robo fainali dhidi ya Ubelgiji. Kiwango hicho ni rekodi katika Fainali za Kombe la Dunia kwa mechi moja tangu (1966-2014).

16: Ni mabao aliyofunga Miroslav Klose katika fainali nne za Kombe la Dunia, hii ni rekodi mpya.

23: Idadi ya wachezaji waliotumiwa na kocha Louis van Gaal katika mechi za Kombe la Dunia 2014 alijitahidi kuwapa wachezaji wake wote nafasi ya kucheza.

30: Sekunde ambazo Clint Dempsey alizitumia kufunga bao katika mechi dhidi ya Ghana, hili ni bao la tano kufungwa mapema katika historia za Kombe la Dunia.

31: Idadi ya Faulo ambazo timu ya taifa ya Brazil ilicheza katika mechi ya robo fainali dhidi ya Colombia; hizo ni faulo nyingi kwa Brazil kufanya katika mechi moja tangu 1966.

32: Mabao ambayo yamefungwa na wachezaji waliotokea benchi katika Fainali za Kombe la Dunia 2014.

43: Ni umri wa kipa wa Colombia, Faryd Mondrago ambaye ameweka historia ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa katika Fainali za Kombe la Dunia.

171: Ni idadi ya mabao yaliyofungwa katika Fainali za Kombe la Dunia 2014, idadi hiyo ya mabao ni sawa na mabao yaliyofungwa katika Fainali za Kombe la Dunia 1998 nchini Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment