
Thursday, 28 August 2014
Friday, 15 August 2014
Sunday, 27 July 2014
Thursday, 24 July 2014
Wednesday, 23 July 2014
Monday, 21 July 2014
TAARIFA ZA UNDANI ZILIZODHIBITISHWA NA SERIKALI YA MAREKANI JUU YA KIFO CHA ALIYEKUWA GAVANA MKUU WA TANZANIA!!
Ballali alilazwa katika hospitali mbili tofauti kabla ya kufariki dunia.
Neville Meena, Mwananchi
Taarifa za Idara za Serikali ya Marekani
zinathibitisha kwamba aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
Daudi Ballali alifariki dunia akiwa Washington DC, akiwa na umri wa
miaka 66.
Gazeti hili lilianza kufanya uchunguzi kuhusu
ukweli wa kifo cha Ballali miaka miwili iliyopita, kutoka na kuwapo kwa
mkanganyiko na sintofahamu kuhusu kifo hicho, vilivyosababishwa na jinsi
alivyoondoka nchini Agosti 2007, kuugua kwake, mazingira ya kifo na
hata usiri uliotawala mazishi yake.
MMOJA AFARIKI DUNIA, WATANO WAJERUHIWA AJALINI TARIME LEO
MTU mmoja, Fatuma Juma Kitumbo (35), amefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali mbaya ya basi la Zakaria Express lenye namba za usajili T 405 CLT lilipoanguka katika eneo la Sen'gensa Kijiji cha Remagwe, Kata ya Nyamaraga, Wilaya ya Tarime mkoani Mara leo.
Marehemu huyo ambaye ni mtoto wa dada yake mpiga picha wa ITV Musoma, Ahmad Kitumbo, alikuwa akitokea nchini Kenya akielekea jijini Mwanza. Imeelezwa kuwa sababu ya kifo chake ni kutokwa na damu nyingi kutokana na ajali hiyo mbaya.
Ajali hiyo ambayo imethibitishwa na Jeshi
la Tarime na Rorya na Kamanda wake Razalo Mambosasa, ilitokea kati ya
saa 2.00 hadi 3.00 asubuhi.
Ilidaiwa kuwa chanzo chake ni dereva wa basi hilo kumkwepa binti mmoja aliyekuwa na ngo'mbe wa kukokotwa na jembe na lori lililokuwa barabarani, ndipo basi hilo likaanguka na kusababisha maafa hayo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri
ya mji wa Tarime, Roberty Onesmo alithibitisha kutokea kwa kifo hicho
na aliwataja majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo kwa matibabu kuwa
ni dereva wa basi hilo Mbaraka Shamsi (35) aliyeumia kifua, Roberty
Nashoni (28) aliyeumia kichwani na mkewe Bhoke Roberty Nashoni (28),
aliyeumia kifuani na kichwani, Selfina Abuo (44), Lucy Ngure (22).
Hata hivyo, alisema Bwana Nashoni na mkewe
wana hali mbaya na wamepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Musoma kuchunguzwa
na kwa matibabu zaidi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilayani hapa,
Amos Sagara Nyabikwi aliwatembelea majeruhi wa ajali hiyo katika
hospitali hiyo na alifanikisha kuwasafirisha majeruhi hao kupelekwa
Hospitali ya Musoma
Subscribe to:
Posts (Atom)