Shirika la Ndege la Flight Link la Dar es Salaam limesema litaanza kutoa huduma ya usafiri wa anga kati ya Dar es Salaam na Iringa muda wowote kuanzia sasa.
Uamuzi wa Flight Link kuanzisha huduma hiyo,
umekuja siku chache baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
kufanya ziara mkoani hapa na kushawishi wadau wa usafiri wa anga kutoa
huduma mkoani hapo.


